Simba Sports Club
News Videos

Queens yafanya mazoezi ya mwisho Abebe Bikila

28 Aug 2024

Nahodha wa timu, Violeth Nicholaus amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho ili kupata nafasi ya tatu.

Violeth amesema malengo yetu yalikuwa kuingia fainali na baadae kutwaa ubingwa lakini kwakuwa imeshindikana kilichobaki ni kupigania kilichopo mbele yetu.

"Tupo tayari kwa mchezo, tunajua itakuwa mechi ngumu kutokana na ubora wa wapinzani lakini tupo tayari."

Advertisement

"Tumeumia kwa kushindwa kuingia fainali lakini tunajua huu ni mpira na sasa tunaangalia kilichopo mbele yetu," amesema Violeth.

Kawempe tulikuwa nao kundi moja na katika mchezo wa hatua ya makundi tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Back to homepage
Share this story