Mchezo huo ulianza kwa kasi huku Simba Queens ikitengeneza nafasi nyingi lakini kikwazo kikawa mlinda mlango wa Fountain Gate.
Queens ilibidi isubiri mpaka dakika ya 86 kupata la kwanza lililofungwa na mlinzi Helana Hamis katika jitihada za kuokoa mpira wa kona uliopigwa na Jentrix Shikangwa.
Aisha Mnunka alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya nne ya nyongeza kipindi cha pili baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Fasila Adhiambo.
Hata hivyo baada ya bao hilo Mnunka alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia hali iliyosababisha kukimbizwa hospitali.
Matokeo haya yanaifanya Simba Queens kufikisha alama 40 na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo.
Mechi ngumu huku Simba Queens wakitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa Kuzitumia