Simba Sports Club
News

Queens yaendelea kutoa dozi TWPL

9 May 2024

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu ambapo Aisha Mnuka alitupatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 42.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ambapo tulipata mabao mawili haraka yote yakifungwa na Jentrix Shikangwa dakika za 58 na 62.

Asha Djafar alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne dakika ya 87 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Bunda.

Advertisement

Kocha Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mwanahamisi Omary, Jentrix Shikangwa na Caroline Rufa na kuwaingiza Asha Djafar, Zainab Mohamed na Zubeda Mgunda.

Queens imefikisha pointi 43 baada ya kucheza mechi 15 ikiwa kileleni mwa msimamo.

Back to homepage
Share this story