Simba Sports Club
News

Queens yaendelea kutoa dozi TWPL

19 Nov 2025

Aisha Mnunka alitupatia bao la kwanza dakika ya 37 baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Elizabeth Joseph.

Wakati kipindi cha pili kikianza benchi la ufundi la Simba Queens lilifanya mabadiliko ya kuwatoa Zawadi Usanase na Zanga Brice na kuwaingiza Elizabeth Wambui na Doto Evarist ambao waliongeza kasi ya mashambulizi.

Jentrix Shikangwa alitupatia bao la pili dakika ya 51 baada ya kumalizia mpira wa kutengwa uliopigwa na Fasila Adhiambo.

Elizabeth Joseph alitupatia bao la tatu dakika ya 65 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Jentrix Shikangwa.

Advertisement

Dakika ya 73 benchi la ufundi la Simba Queens lilifanya mabadiliko ya kumtoa mlinzi Emeliana Mdimu aliyepata maumivu na kumuingiza Neema Mtunzi.

Dakika ya 83 Simba Queens ilifanya mabadiliko ya wachezaji wengine wawili ambapo Fasila Adhiambo na Elizabeth Joseph walitoka nafasi zao zikachukuliwa na Elizabeth Nashon na Cordelia Amarachi.

Ushindi huo unaifanya Simba Queens kufikisha alama sita wakiwa wamefunga mabao saba huku wakiwa hawajaruhusu bao na kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi.

Back to homepage
Share this story