Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini nafasi zilizotengenezwa zikiwa hazijatumiwa vizuri.
Licha ya kosa kosa za hapa na pale milango yote ilikuwa migumu na timu zilienda mapumziko bila kufungana.
Advertisement
Zawadi Usanase alitupatia bao hilo pekee dakika ya 60 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja akiwa nje ya 18.
Ushindi huo umeifanya Queens kufikisha alama 12 ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya kushinda mechi zote nne za Ligi ilizocheza.