Simba Sports Club
News

Queens yaendelea kujikita kileleni mwa WPL

8 Apr 2026

Jentrix Shikangwa alitupatia bao la kwanza dakika ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Fasila Adhiambo.

Dakika ya 30 Fasila alitupatia bao la pili baada ya shuti lililopigwa na Jentrix kugonga mwamba kabla ya kumkuta mfungaji.

Kipindi cha pili kocha mkuu, Mussa Hassan Mgosi alifanya madadiliko ya kuwatoa Esther Mayala, Vivian Corazone, Elizabeth Wambui na Emiliana Mdimu na kuwaingiza Elizabeth Joseph, Zawadi Usanase, Fatuma Issa na Dotto Evarist.

Advertisement

Zawadi Usanase alitupatia bao la tatu dakika ya 85 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na walinzi wa Bunda wakachelewa kuondoa kwenye hatari.

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 37 baada ya kucheza mechi 13 tukishinda 12 na kutoka sare moja pekee.

Back to homepage
Share this story