Simba Sports Club
News

Queens yaanza mzunguko wa pili kwa kishindo

3 Apr 2026

Pamoja na kumiliki mchezo muda mrefu na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Bilo lakini Simba Queens ilibidi wasubiri mpaka dakika ya 40 kupata bao la kwanza lililofungwa na mlinzi wa kati Ruth Ingosi.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zilivyooenda mapumziko ingawa bado tuliendelea tumiliki sehemu kubwa.

Jentrix Shikangwa alitupatia bao la pili dakika ya 58 baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 kufuatia walinzi wa Bilo kuchelewa kumdhibiti.

Simba Queens ilipata mabao mengine mawili ya haraka haraka kupitia kwa Aisha Mnunka na Zainah Nandede na kutufanya kuwa mbele kwa 4-0.

Advertisement

Fasila Adhiambo alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la tano dakika ya 90 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja na kutuhakikishia alama tatu muhimu ugenini.

Kocha Mkuu Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Fatuma Issa, Elizabeth Nashon Jentrix Shikangwa na kuwaingiza Elizabeth Nashon, Esther Mayala na Zainah Nandede.

Baada ya ushindi huu Queens imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo kwa kufikisha alama 34 baada ya kucheza mechi 12.

Back to homepage
Share this story