Queens ilianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango la Ceasiaa ambao muda mwingi walikuwa wakizuia.
Katika ushindi huo mshambuliaji Aisha Juma amefunga mabao matatu 'hat trick' nakuwa mwiba mchungu kwa walinzi wa Ceasiaa.
Advertisement
Mabao mengine ya Queens yaliwekwa kambani na Asha Djafar na Mwanahamisi Omary aliyeingia kipindi cha pili.
Kocha Mkuu Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Violeth Nicholas, Asha Rashid, Ruth Ingosi na Vivian Corazone na kuwaingiza Koku Kipanga, Mwanahamisi Omary, Fatuma Issa, Joanitah Ainebambazi na Joelle Bukuru.