Queens inayonolewa na Kocha,l Sebastian Nkoma, imefikisha pointi 57 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ikiwa imebakiwa na mechi mbili.
Katika mchezo huo uliokuwa mgumu wenye upinzani mkubwa tulipata bao la kwanza kupitia kwa Asha Djafar kwa mkwaju wa penati dakika ya 31 kabla ya Mlandizi kusawazisha dakika ya 38 lililofungwa na Victoria.
Advertisement
Silvia Mwacha alitupatia bao la ushindi dakika ya 67 na kutuhakikisha ubingwa wetu wa tatu mfululizo wa michuano hii.
Kocha Nkoma alifanya mabadiliko mara moja tu ya kumtoa Amina Ramadhani na kumuingiza Olaiya Barakat.