Simba Sports Club
News

Queens kuondoka kesho kuifuata Bilo

30 Mar 2026

Queens itacheza mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi ya Wanawake Aprili 3 dhidi ya Bilo Queens utakaopigwa katika Uwanja wa Nyamagana.

Mchezo wa pili utakuwa dhidi ya Bunda Queens ambao utapigwa katika Uwanja wa Karume Aprili 8.

Advertisement

Queens itaondoka na kikosi cha wachezaji 24 tayari kwa michezo hiyo miwili kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.

Simba Queens inarejea kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Wanawake ikiwa na alama 31 kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 11 ikishinda 10 na kutoka sare moja.

Back to homepage
Share this story