Mchezo huo ambao utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote utapigwa Agosti 24 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Queens itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi zote tatu za hatua ya makundi na kufanikiwa kufunga mabao 11 bila kuruhusu bao lolote.
Advertisement
Lengo la kwanza ni kuhakikisha tunashinda michuano hii katika ardhi ya nyumbani na kuiwakilisha Afrika Mashariki na Kati kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.