Simba Sports Club
News

Queens kuivaa Ceasiaa Samora Kesho

4 Nov 2024

Queens imewasili Iringa tangu jana na leo kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Samora tayari kwa mchezo huo utakaonza saa 10 jioni.

Wachezaji wote waliosafiri na timu wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Advertisement

Queens itaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-1 iliyopata dhidi ya Fountain Gate Princess kwenye mechi iliyopigwa na Oktoba 14.

Queens ndio vinara wa Ligi Kuu ya Wanawake ikiwa na alama sita ikifunga mabao sita na kuruhusu moja katika mechi mbili.

Back to homepage
Share this story