Simba Sports Club
News

Queens kucheza mechi ya mshindi wa tatu Jumamosi

10 Nov 2022

Queens ambayo imeweka historia yakuwa timu ya kwanza kutoka Afrika Mashariki kutinga nusu fainali ya michuano hiyo jana tumepoteza kwa bao moja dhidi ya mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns.

Baada ya mchezo wa jana wachezaji wamepumzika kwa saa chache na leo jioni wataanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo muhimu.

Advertisement

Lengo letu lilikuwa ni kufika fainali ya michuano hii mikubwa Afrika lakini baada ya kushindikana tunahitaji kupata ushindi Jumamosi ili tuichukue nafasi ya tatu.

Tunajua mchezo utakuwa mgumu na tunaiheshimu Bayelsa lakini tumejipanga madhubuti kwa ajili ya kuhakikisha tunashinda.

Back to homepage
Share this story