Queens itaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa kinara kwenye msimamo baada ya kufikisha pointi 19.
Queens itaingia katika mchezo wa kesho ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mnono wa mabao 4-1 tuliopata dhidi ya Baobab Queens katika mechi iliyopita.
Advertisement
Maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri wachezaji wapo kwenye hali nzuri na baada ya kukaa kileleni kwa msimamo lengo ni kuhakikisha hatushuki hadi tutetee ubingwa wetu.
Ingawa Ceasiaa haipo juu au sio miongoni mwa timu zinazowania taji lakini tutaingia kwa kuiheshimu na kuhakikisha tunatumia vizuri nafasi tutakazopata.