Simba Sports Club
News

Queens, JKT hakuna mbabe SLWPL

9 Mar 2023

Katika mchezo huo uliokuwa mzuri wa kuvutia timu zote zikishambuliana kwa zamu huku zikipoteza nafasi nyingi za kufungana.

Timu zilikuwa zikipokezana umiliki wa mchezo huku ukionogeshwa na umahiri wa mchezaji mmoja mmoja wa pande zote.

Wenyeji JKT walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 41 lililofungwa na Donesia Minja baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zinaenda mapumziko ingawa kulikuwa na mashambulizi kadhaa lakini hayakuweza kubadili ubao wa matokeo.

Advertisement

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na ilituchukua dakika nane kusawzisha bao hilo kupitia kwa Jentrix Shikangwa baada ya shuti lililopigwa na Asha Mnuka kuokolewa na mlinda mlango wa JKT kabla ya kumkuta mfungaji.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa wachezaji wawili Danai Bhobho na Pambani Kuzoya na kuwaingiza Joelle Bukuru na Asha Rashid.

Sare hii inatufanya kufikisha pointi 23 baada ya kucheza mechi 10 tukiendelea kushika usukani.

Back to homepage
Share this story