Simba Sports Club
News

Queens ipo tayari kuivaa Bunda Queens Kesho

21 Jan 2024

Mgosi amesema wachezaji wote tuliosafiri nao wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa kesho na wamefanya mazoezi ya mwisho leo.

Mgosi ameongeza kuwa tunategemea kupata ugumu mkubwa kutoka kwa Bunda lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi zote tatu.

Advertisement

Kikosi chote kiko tayari tulifika salama hapa Musoma juzi, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini sisi tubahitaji alama tatu na kila mchezo kwetu ni fainali tunaamini tutashinda kesho," amesema Mgosi.

Simba Queens ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi baada ya kufikisha pointi 12 tukishinda mechi zote nne za kwanza.

Back to homepage
Share this story