Simba Sports Club
News

Queens ipo Kamili kuivaa Yanga Princess kesho

27 Dec 2025

Mgosi amesema maandalizi yote yamekamilika na wachezaji wameandaliwa kimwili na kiakili kwa ajili ya mchezo ambao tunategemea utakuwa mgumu.

Mgosi ameongeza kuwa mchezo dhidi ya Yanga una upinzani mkubwa ndani na nje ya uwanja hivyo tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi ili kufikia malengo tuliyojiwekea.

"Tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho dhidi ya Yanga Princess, mara zote mechi hii huwa ngumu. Kuna upinzani mkubwa kati ya timu na timu, makocha mpaka mashabiki ndio maana tumejipanga kushinda ili kuwapa furaha Wanasimba wote," amesema Mgosi.

Advertisement

Kwa upande wake nahodha wa timu, Vivian Corazone amesema wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na walimu ili kuhakikisha alama tatu zinapatikana.

"Malengo yetu katika kila mechi ni kupata alama tatu, tunaenda kukutana na Yanga ambayo ni timu kubwa kama sisi na tunafahamu tutapata upinzani mkubwa lakini ili uwe mkubwa lazima ufunge timu kubwa kwahiyo tumejipanga ili kufikia malengo tuliyojiwekea," Vivian Corazone, nahodha wa Simba Queens.

Back to homepage
Share this story