Abdulnasir amesema mchezo wa kesho hauhitaji pointi bali ushindi ili kusonga mbele hivyo wachezaji wameandaliwa kuhakikisha malengo yanafikiwa.
Abdulnasir ameongeza kuwa kikosi chetu kina idadi kubwa ya wachezaji wapya lakini hiyo haitakuwa changamoto kwakuwa muda wa maandalizi umepatikana wa kutosha.
"Mchezo wa kesho unahitaji ushindi pekee ili kufuzu hatua inayofuata, tumewaandaa vizuri wachezaji kimwili na kiakili kuhakikisha tunapata ushindi," amesema kocha Abdulnasir.
Nae nahodha wa timu, Esther Mayala amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kuhakikisha wanapambana ili kufikia malengo ya kutinga fainali na baadae kutwaa taji.
"Ni jambo la wazi kuwa tunahitaji ushindi kwenye mchezo wa kesho ingawa haitakuwa mechi rahisi. Tunajua mpira ni mchezo wa makosa lakini tumejiandaa na tupo tayari kwa ajili ya kupambana," amesema Esther.