Simba Sports Club
News

Queens iko tayari kwa Fainali ya CECAFA kesho

26 Aug 2022

Nkoma amesema lengo la kwanza ni kuhakikisha tunashinda na kuchukua ubingwa kuwapa furaha mashabiki wetu na kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nkoma ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu na anaamini SHE Corporates watakuja kivingine hasa baada ya kuwafunga katika mchezo wa hatua ya makundi.

"Kikosi kipo tayari morali kwa wachezaji ipo juu, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ili kuchukua ubingwa," amesema Nkoma.

Advertisement

Kwa upande wake mshambuliaji Aisha Juma amesema wao kama wachezaji wapo kamili ingawa wanafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini lengo ni moja kuchukua ubingwa.

Naye kiungo fundi Joelle Bukuru, amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kutupa sapoti huku akiwaahidi kuwapa furaha.

"Sisi tupo tayari tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kushinda kikubwa tunahitaji mashabiki waje kwa wingi uwanjani kutupa sapoti," amesema Joelle.

Back to homepage
Share this story