Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini umakini wa kumalizia nafasi zilizopatikana ikawa changamoto.
Mlinzi wa kati Juliet Singano alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya nne baada ya kumchezea faulo Clara Luvanga.
Clara aliwapatia bao hilo Yanga Princess dakika ya 45 baada ya kupiga shuti ambalo lilimgonga mlinda mlango wetu Gelwa Yona kabla ya kuingia wavuni.
Advertisement
Kipindi cha pili tuliongeza kasi kutafuta bao la kusawazisha lakini bahati haikuwa upande wetu kutokana na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga.
Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Jackline Albert, Wema Richard na Asha Djafar na kuwaingiza Amina Ramadhani, Koku Kipanga na Mercy Tagoe.