Simba Sports Club
News

Phiri Mchezaji Bora wa Mashabiki Septemba

3 Oct 2022

Phiri ameshinda kinyang'anyiro hicho baada ya kuwashinda nyota wawili ambao ni viungo Clatous Chama na Mzamiru Yassin ambao aliingia nao fainali.

Katika mwezi Septemba Phiri amecheza mechi nne akifunga mabao matatu na kusaidia mengine mawili baada ya kucheza dakika 334.

Mchanganuo wa kura zilivyopigwa

Kura Asilimia

Phiri 3564 73.97

Advertisement

Chama 1089 22.60

Mzamiru 165 3.42

Kwa kushinda tuzo hiyo Phiri atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Phiri anakuwa mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo msimu huu katika kikosi chetu baada ya Chama kufanya hivyo mwezi Agosti.

Back to homepage
Share this story