Simba Sports Club
News

Phiri, Kyombo kuongoza mashambulizi dhidi ya Eagle leo

10 Dec 2022

Mgunda amewaanzisha Moses Phiri na Habib Kyombo kuongoza mashambulizi huku Nahodha John Bocco akianzia benchi.

Wawili hao watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama na Pape Sakho.

Kocha Mgunda pia amewaanzisha walinzi wa kati Kennedy Juma na Mohamed Ouattara wakichukua nafasi za Henock Inonga na Joash Onyango ambao wamekuwa wakianza mara nyingi.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Advertisement

Beno Kakolanya (30), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Habibu Kyombo (32), Moses Phiri (25), Pape Sakho (10).

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Erasto Nyoni (18), Nassor Kapama (35), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Nelson Okwa (8), John Bocco (22), Kibu Denis (38), Augustine Okrah (27).

Back to homepage
Share this story