Simba Sports Club
News

Phiri: Kusafiri na Mashabiki kwenda Ndola kunatupa hamasa wachezaji

11 Sep 2023

Phiri amesema mashabiki wana nafasi kubwa ya kuifanya timu kufanya vizuri kwakuwa mara zote wachezaji wanajiona wana deni kwao.

"Tunafurahi kuona tunasafiri na mashabiki kutoka Dar es Salaam, hii itakuwa chachu kubwa kwetu kuhakikisha tunapambana kuwapa furaha mashabiki ambao wametoka nyumbani kuja kutupa sapoti sisi," amesema Phiri.

Akizungumzia mchezo wenyewe Phiri amesema "itakuwa mechi ngumu, Dynamos ni timu bora na ipo nyumbani ukizingatia siku chache zilizopita tumecheza nao kwahiyo tunafahamiana vizuri."

Advertisement

Phiri ambaye tumemsajili kutoka Zanaco ameongeza kuwa kuna kumbukumbu nyingi kila mara anaporudi kucheza nyumbani kwao Zambia hasa anapokutana na Power Dynamos.

"Kumbukumbu zipo nimewahi kucheza dhidi ya Power Dynamos, nafurahi kucheza kwenye ardhi ya nyumbani lakini nipo tayari kuipigania timu yangu ya Simba kupata ushindi," amemalizia Phiri.

Back to homepage
Share this story