Simba Sports Club
News

Phiri afunguka siri ya kufunga kila mechi, amtaja Chama

19 Sep 2022

Katika mabao manne tuliyopata kwenye mechi mbili dhidi ya Nyasa Big Bullets katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Phiri amefunga matatu.

Phiri pia amezungumzia maelewano makubwa 'patnashipu' aliyo nayo na kiungo mshambuliaji Clatous Chama ndani ya uwanja kuwa ni mazuri huku akimuita 'Master'.

Advertisement

"Siri ya mafanikio ni kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzangu pamoja na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

"Kuhusu Chama huyu ni master anajua kutoa pasi katika nafasi ambayo mshambuliaji anasubiri, ndiyo maana wanamuita Mwamba wa Lusaka," amesema Phiri.

Back to homepage
Share this story