Phiri alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumizwa na alipata huduma ya kwanza huko Kagera na alipofika jijini Mwanza akapelekwa moja kwa moja hospitali.
Daktari wa timu Edwin Kagabo, amesema kwa sasa hawezi kuzungumzia hali ya mshambuliaji huyo mpaka atakapopata majibu ya vipimo kutoka hospitali.
Advertisement
"Phiri alipata maumivu katika mchezo uliopita na amefanyiwa vipimo vya MRI na tunasubiri majibu yatoke ili tujue ukubwa wa jeraha ndipo sasa tunaweza kuzungumzia hali yake," amesema Dk. Kagabo.