Simba Sports Club
News

Phiri aahidi makubwa baada ya kurejea uwanjani

1 Feb 2023

Phiri amesema ushindani wa namba umekuwa mkubwa baada ya kuongezwa wachezaji wapya lakini nitapambana kurudisha nafasi yangu.

"Nina furaha nimerudi, sio kitu kizuri kwa mchezaji kukosa mechi nyingi kutokana na majeruhi lakini nimejipanga kuhakikisha narudi kwa nguvu kama nilivyoanza msimu.

Advertisement

"Kwa sasa niko fiti baada ya mchezo dhidi ya Singida nitakuwa tayari kucheza, nimejipanga kuhakikisha naendeleza ubora wangu.

Akizungumzia kuhusu ujio wa mshambuliaji, Jean Baleke, Phiri amesema "ni mchezaji mzuri, ana kasi pia anajua kufunga naamini ataisaidia timu."

Back to homepage
Share this story