Simba Sports Club
News

Pambani Mchezaji bora wa mechi

2 Nov 2022

Pambani ameonyesha kiwango bora kwenye mchezo huo ambao tumeibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kurejesha matumaini ya kutinga nusu fainali.

Kipindi cha pili baada ya kocha Charles Lukula kufanya mabadiliko ya kumtoa Vivian Corazone ilimfanya Pambani kushuka chini kucheza pamoja na Joelle Bukuru ambapo aliifanya safu yetu ya kiungo kuwa imara tukizuia na kushambulia kwa pamoja.

Advertisement

Baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi Pambani amewashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano mkubwa waliompa hadi kufanikisha jambo hilo.

"Nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano walionipa, pia benchi la ufundi kwa kunipa nafasi ya kucheza naamini tutaendelea kufanya vizuri," amesema Pambani.

Back to homepage
Share this story