Simba Sports Club
News

Pambani Mchezaji bora wa mechi

2 Nov 2022 By simbasc 354 views
Kiungo mshambuliaji Pambani Kuzoya amechaguliwa mchezaji bora wa mechi yetu dhidi ya Determine Girls kutoka Libya katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Pambani ameonyesha kiwango bora kwenye mchezo huo ambao tumeibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kurejesha matumaini ya kutinga nusu fainali. Kipindi cha pili baada ya kocha Charles Lukula kufanya mabadiliko ya kumtoa Vivian Corazone ilimfanya Pambani kushuka chini kucheza pamoja na Joelle Bukuru ambapo aliifanya safu yetu ya kiungo kuwa imara tukizuia na kushambulia kwa pamoja. Baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi Pambani amewashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano mkubwa waliompa hadi kufanikisha jambo hilo. "Nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano walionipa, pia benchi la ufundi kwa kunipa nafasi ya kucheza naamini tutaendelea kufanya vizuri," amesema Pambani.
Advertisement
Back to homepage
Share this story