Simba Sports Club
News

Pablo: Ushindi dhidi ya ASEC ni muhimu sana kwetu

14 Feb 2022

Pablo amesema michuano ya Afrika mara zote ni vizuri kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani ili ugenini ukipata hata sare inakuweka katika hali nzuri.

Akizungumzia mchezo wenyewe, Pablo amesema ulikuwa mgumu na wa kimbinu lakini tulikuwa bora zaidi yao kwenye kutengeneza nafasi na kumiliki mpira.

Advertisement

Pablo ameongeza kuwa tulikuwa na nafasi ya kupata ushindi mnono zaidi kama tungezitumia vizuri nafasi za wazi tulizopata kipindi cha kwanza ingawa hata hivyo amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya.

"Ni ushindi muhimu tumepata, tulicheza vizuri, tulitengeneza nafasi na tulikuwa na uwezo wa kushinda zaidi ya mabao tuliyopata. Kwanza niwapongeze wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya, haikuwa rahisi," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story