Pablo amesema tunaenda kukutana na timu ngumu ambayo ilitufunga kwao hivyo nasi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunapata ushindi katika uwanja wa nyumbani.
Pablo ameongeza kuwa tumekuwa na wiki nzuri ya mazoezi na wachezaji wengi waliokuwa majeruhi wamerejea kikosini na wameongeza nguvu kuelekea mchezo wa kesho.
Advertisement
"Tupo katika uwanja wa nyumbani tunahitaji kupata alama tatu. Tunaenda kukutana na timu bora ambayo ilitufunga kwao lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda kwetu.
"Tumepata muda mzuri wa kujiandaa, tulikuwa na wiki ya kufanya mazoezi wachezaji wapo kwenye hali nzuri tunaamini tutafanya vizuri kesho," amesema Pablo.