Simba Sports Club
News

Pablo: Tunaelekeza nguvu zetu kwenye Ligi

1 Mar 2022

Pablo amesema tuna michezo miwili ya ligi inayofuatana dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji kabla ya kurudiana na RS Berkane katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hivyo tunapaswa kuhakikisha tunashinda yote.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Biashara utakaopigwa Ijumaa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Pablo amesema utakuwa mgumu kutokana na uimara wa wapinzani hasa wanapokutana na timu kubwa.

"Biashara ni timu nzuri, incheza kitimu pia ina wachezaji wazuri mmoja mmoja. Inapocheza na timu kubwa inatoa upinzani mkubwa lakini tutahakikisha tunapambana kupata ushindi uzuri ni kuwa tupo nyumbani na tutakuwa mbele ya mashabiki wetu," amesema Pablo.

Advertisement

Kwa upande wake Nahodha John Bocco amesema akili za wachezaji wamezihamishia katika mechi hizobmbili za ligi kwanza kabla ya kukutana na Berkane.

"Tumerudi nyumbani tumeona tofauti ya pointi dhidi ya wanaoongoza ligi ni kubwa, tunahitaji kushinda ili kuendelea kuzipunguza na kuwapa presha vinara na kutimiza lengo la kutetea ubingwa wetu," amesema Bocco.

Back to homepage
Share this story