Simba Sports Club
News

Pablo: Tumekuja kuvunja mwiko wa ASEC

19 Mar 2022

Pablo amekiri ASEC ni timu nzuri na wanaweza kufanya chochote hasa wakiwa nyumbani lakini tumekuja kuhakikisha tunabadili historia hiyo.

Pablo ameongeza kuwa matokeo ya ushindi katika mchezo wa kesho yatatuhakikishia kuingia robo fainali ya michuano hii na ndiyo lengo letu la kwanza.

Advertisement

"ASEC ni timu nzuri wametuonesha walivyokuja Dar es Salaam lakini pia katika kundi letu wao wana uwezo wa kufanya chochote lakini tumejipanga kuhakikisha tunawadhibiti.

"Tumekuja kupambana kubadili historia yao ya kutofungwa nyumbani tunataka kuwa wa kwanza kuwafunga ASEC kwao," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story