Simba Sports Club
News

Pablo: Tumejipanga ndani na nje ya uwanja ili tufuzu nusu fainali

22 Apr 2022

Pablo ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili Afrika Kusini mchana huu tayari kwa mchezo huo wa Jumapili ambao tutapambana kufa na kupona ili kuhakikisha tunafanikiwa kufuzu.

Pablo amesema tunajua tutakutana na mazingira tofauti kwa kuwa wenyeji watajaza uwanja na kushangiliwa lakini tumeweka mpango kazi kuhakikisha jambo hilo halitusumbui.

Pablo ameongeza kuwa kiungo mkabaji Sadio Kanoute na mlinzi wa kati Joash Onyango watakuwa sehemu ya kikosi baada ya kumalizia kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano huku Bernard Morrison akiachwa nyumbani.

Advertisement

"Tumekuja tukiwa tunajua mchezo utakuwa mgumu. Orlando watakuja kwa kasi kutushambulia pia hali ya uwanja itakuwa msaada kwao lakini tumejipanga kuwakabili kwa kila hali.

"Tunajua pia hatufanyi vizuri kwenye mechi za ugenini lakini ni muda wa kubadili mtazamo huu kwa kuhakikisha tunashinda na kutinga nusu fainali," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story