Simba Sports Club
News

Pablo: Hakuna timu rahisi, tutapanga kikosi Kamili

13 May 2022

Pablo amesema ni mchezo muhimu na tunahitaji kushinda ili kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano na hatimaye tutetee taji letu.

Pablo ameongeza kuwa tutachukua tahadhari zote na hutataidharau Pamba kwakuwa ipo Championship, tumeupa umuhimu mkubwa mchezo wa kesho.

Advertisement

"Katika michuano hii hakuna timu rahisi, huu ni mchezo muhimu kwetu tunahitaji kushinda ili kusonga mbele. Tutapanga kikosi kamili kwa wachezaji wote walio tayari kwa mchezo.

"Nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu, tunahitaji kupata ushindi," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story