Simba Sports Club
News

Pablo awavulia kofia mashabiki

5 Dec 2021

Kocha Mkuu Pablo Franco, amewasifu mashabiki wetu waliosafiri kutoka nchini Tanzania hadi Zambia kwa ajili ya kuisapoti timu kufanya vizuri.

Pablo amefurahishwa na mapenzi makubwa waliyoonyesha mashabiki hao huku akiweka wazi mafanikio tuliyopata ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ni kwa ajili yao.

Amesema idadi kubwa ya mashabiki waliofika uwanjani waliongeza hamasa kwa wachezaji kupambana muda wote wa mchezo na kufanikisha kufuzu hatua hiyo.

Advertisement

"Nawashukuru mashabiki waliosafiri kutoka Dar es Salaam na wale tuliowakuta huku Zambia, wamefanya kazi kubwa ya kutoa hamasa kwa wachezaji. Ilikuwa inafurahisha kuwaona wakishangilia.

"Tangu jana wakati tunafanya mazoezi walijitokeza kwa wingi, walikuja hadi hotelini kuonana na wachezaji ili kuwapa hamasa. Mafanikio haya ya kuingia hatua ya makundi ni kwa ajili yao," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story