Licha ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, Kocha Mkuu Pablo Franco amewasifu wachezaji kwa jinsi walivyojituma muda wote.
Pablo amesema ingawa uwanja haukuwa rafiki kwa wachezaji wetu na aina ya soka tunalocheza lakini walipambana muda wote kuhakikisha tunapata ushindi ingawa haikuwa bahati yetu.
Kocha huyo ameongeza kuwa tulitengeneza nafasi hasa kipindi cha pili ambazo tungeweza kuzitumia na kupata mabao kama ile ya dakika ya mwisho ya mlinzi Shomari Kapombe.
"Pamoja na kuwa uwanja haukuwa rafiki kwa wachezaji na aina soka tunalocheza lakini walipambana muda wote kutafuta ushindi, nimependa jinsi walivyojitoa kwa timu.
"Tumekuwa tukicheza mechi karibu karibu, wachezaji wanaumia lakini hakuna jinsi tunapaswa kucheza. Tunarudi Dar es Salaam tutapata siku moja ya mazoezi kabla ya kusafiri kwenda Kagera," amesema Pablo.