Simba Sports Club
News

Pablo awapongeza wachezaji ushindi dhidi ya Pamba

15 May 2022 By simbasc 682 views

Kocha Mkuu Pablo Franco, amewasifu wachezaji baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba FC na kufanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Pablo amesema ilikuwa mechi nzuri ambayo tuliitawala kwa kiasi kikubwa ambayo kama tungeongeza umakini tungepata ushindi mnono zaidi.

Advertisement

Pablo ameongeza kuwa kipindi cha kwanza tulipoteza nafasi nyingi za kufunga lakini hakutuzitumia vizuri lakini mabadiliko tuliyofanya yalituwezesha kupata ushindi huo mnono.

"Kwanza niwapongeze wachezaji kwa ushindi huu, ni jambo jema tumefuzu nusu fainali. Mchezo ulikuwa mzuri lakini tuliokuwa na nafasi ya kupata ushindi mnono zaidi," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story