Simba Sports Club
News

Pablo atoa neno kuelekea mechi dhidi ya ASEC

12 Feb 2022

Pablo amesema kumekuwa na changamoto ya kupata mabao licha ya kutengeneza nafasi nyingi lakini tayari suala hilo limefanyiwa kazi mazoezini na kila kitu kiko sawa.

Akizungumzia mchezo wenyewe Pablo amesema utakuwa mgumu kutokana na ubora wa ASEC pamoja uzoefu wao lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda katika uwanja wa nyumbani.

Advertisement

"Ninaamini tutaanza kupata mabao mengi, tumekuwa tukifanya mazoezi sana kuhusu ufungaji na kila kitu kitakaa sawa kuanzia kesho," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story