Simba Sports Club
News

Pablo ataja siri ya ushindi mnono dhidi ya Ruvu Shooting

17 Feb 2022

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema mchezo mzuri wa viwango dhidi ya Ruvu Shooting leo ambapo pia tulicheza vizuri na kuhakikisha tunatumia nafasi tulizopata na hicho ndicho kilichopelekea ushindi mnono wa mabao 7-0.

Pablo amesema tulipata bao la mapema kabla ya kuongeza mengine manne na kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 5-0 na kusabaisha wachezaji wetu wacheze kwa kujiamini.

Pablo ameongeza kuwa ushindi wa leo umerejesha morali kwa wachezaji na matumaini ya kuendelea kushinda ni makubwa kwakuwa timu imeanza kuzoeana.

Advertisement

"Tulicheza vizuri muda mrefu, tulikuwa na nafasi ya kupata mabao mengi zaidi kipindi cha kwanza na hilo ni jambo zuri.

"Ushindi huu umeongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji na utulivu umeongezeka naamini tutaendelea kupata ushindi mnono katika mechi zetu zinazofuata," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story