Simba Sports Club
News

Pablo anena ushindi dhidi ya Orlando

18 Apr 2022

Pablo amesema michuano ya Afrika ni migumu hivyo unapaswa kutumia vema uwanja wa nyumbani ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye mchezo wa marudiano.

Pablo ameongeza kuwa tunatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Orlando kwenye mchezo wa marudiano lakini tutajipanga kuhakikisha tunaenda kufanya vizuri ugenini.

Advertisement

Pablo amekiri kuwa hatukuwa na matokeo mazuri kwenye mechi za ugenini katika hatua ya makundi kwa hiyo tunapaswa kujipanga hasa kutokana na ubora wa wapinzani.

"Michuano ya Afrika mara nyingi timu zinafanya vizuri nyumbani kama tulivyofanya. Tutajipanga kuelekea mchezo wa marudiano ugenini tunahitaji kufuzu nusu fainali," amesema Pablo.

Back to homepage
Share this story