Kocha Mkuu Pablo Franco amesema alama moja tuliyopata katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania haitoshi kutokana na idadi ya pointi tulizoachwa na wanaoongoza ligi.
Pablo amesema matokeo ya sare si mazuri kwetu sababu malengo yetu ni kutetea ubingwa wa ligi hivyo tulipaswa kukusanya alama tatu.
Hata hivyo, Pablo ameainisha sababu za kukosa alama tatu katika mchezo huo ni kutokana na ubovu wa eneo la kuchezea (pitch) huku pia tukikosa maandalizi kutokana na ugumu wa ratiba.
"Si matokeo mazuri kwetu, tulipaswa kushinda kutokana idadi kubwa ya pointi tulizoachwa na malengo yetu bado ni kutetea ubingwa.
"Sitaki kuongelea kuhusu ugumu wabratiba kwa kuwa kama unacheza mechi mfululizo katika viwanja ambavyo si vizuri na wachezaji hawapumziki hili lazima lingetokea," amesema Pablo.