Pablo amesema licha ya uwanja kutokuwa rafiki kwa aina soka tunalocheza lakini tulijitahidi kucheza kwenye mipango yetu mpaka kupata ushindi huo.
Pablo amesema tulistahili kupata ushindi mnono zaidi kama tungetumia vizuri nafasi tulizotengeneza lakini tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo.
Raia huyo wa Hispania amesema hatuna muda wa kupumzika wala kujiandaa badala yake tunapaswa kusafiri kuelekea mkoani Kilimanjaro tayari kwa mchezo ujao dhidi ya Polisi Tanzania.
"Nimefurahi kupata alama tatu za ugenini, huu ni ushindi muhimu kwetu, tulicheza vizuri ingawa uwanja haukuwa rafiki lakini tulicheza katika mipango yetu.
"Tulistahili kupata mabao zaidi kama tungetumia vizuri nafasi tulizotengeneza. Hatuna muda wa kujiandaa tunapaswa kusafiri kwa ajili ya mchezo wetu unaofuata," amesema Pablo.