Simba Sports Club
News

Pablo afunguka kuhusu Derby kesho

27 May 2022

Pablo amesema ushindi katika mchezo wa kesho utaongeza ari kuelekea kukamilisha msimu na tutakuwa tumekaa katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa michuano hii.

Pablo ameongeza wachezaji wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho na kila mmoja anajua anachotakiwa kukifanya akipewa nafasi ya kucheza.

"Itakuwa mechi ngumu, tupo kwenye hatua ya nusu fainali na ni mchezo wa Derby lazima uwe na msisimko lakini tupo tayari kwa mapambano. Tunahitaji sana kupata ushindi katika mchezo wa kesho," amesema Pablo.

Advertisement

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi, Shomari Kapombe amesema kwa upande wao wachezaji wamepata maandalizi ya kutosha na wapo tayari kwa mchezo wa kesho.

"Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho. Tunajua utakuwa mgumu, tumetoka sare kwenye mechi mbili zilizopita msimu huu na kesho ni nusu fainali hivyo tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuingia fainali," amesema Kapombe.

Back to homepage
Share this story