Simba Sports Club
News

Pablo abadili watano dhidi ya Pamba Leo

14 May 2022 By simbasc 710 views

Kocha Mkuu Pablo Franco amefanya mabadiliko ya wachezaji watano katika kikosi kitakachoshuka dimbani leo kuikabili Pamba FC katika mchezo wa robo fainali ya Azam Sports Federation Cup ASFC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Pablo amewaanzisha mlinda mlango Beno Kakolanya walinzi Jimmyson Mwanuke na Kennedy Juma pamoja na mawinga Peter Banda na Yusuf Mhilu ambao hawakuanza katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.

Nahodha John Bocco ataongoza mashambulizi kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita huku akipata msaada wa karibu kutoka kwa Kibu Denis na Rally Bwalya.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Advertisement

Beno Kakolanya (30), Jimmyson Mwanuke (21), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Mzamiru Yassin (19), Peter Banda (11), Rally Bwalya (8),John Bocco (22), Kibu Denis (38),
Yusuf Mhilu (27).

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Gadiel Michael (2), Henock Inonga (29), Taddeo Lwanga (4), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14)

Back to homepage
Share this story