Pablo amewapanga mabeki watatu wa kati badala ya wawili kama ilivyozoeleka. Mabeki hao ni Joash Onyango, Henock Inonga pamoja na Pascal Wawa.
Katika eneo la kiungo wa ulinzi amewapanga Jonas Mkude na Sadio Kanoute huku Shomari Kapombe aliyepangwa kama winga wa kulia atakuwa anaingia kati pia kuongeza idadi ya viungo.
Mshambuliaji Chris Mugalu ataongoza mashambulizi akipata msaada wa karibu kutoka Pape Ousmane Sakho.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Israel Patrick (5),
Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Henock Inonga (29), Shomari Kapombe (12), Jonas Mkude (20), Chris Mugalu (7), Sadio Kanoute (13), Pape Sakho (17)
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19), Peter Banda (11), Taddeo Lwanga (4), Rally Bwalya (8), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38)