Simba Sports Club
News

Ouattara arejea mazoezini

24 Mar 2023

Ouattara alipata majeraha akiwa mazoezini wakati wa maandalizi ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya kutoka Guinea wiki iliyopita ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 7-0.

Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema Ouattara alipata maumivu ya nyama za paja lakini sasa anaendelea vizuri na leo ameanza mazoezi.

Advertisement

Dk. Edwin amesema Ouattara ataendelea kufanya mazoezi chini ya uangalizi wa daktari kwa siku tatu kabla ya kuruhusiwa kujiunga moja kwa moja na wenzake.

"Ouattara alipata majeraha ya nyama za paja leo ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi na baada ya siku tatu ataruhusiwa kujiunga na wenzake," amesema Dk. Edwin.

Back to homepage
Share this story