Katika michuano hiyo Opa ameisaidia Queens kufika nusu fainali huku akifunga mabao mawili akichaguliwa mchezaji bora wa mechi mara moja (Woman of the match).
Katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Green Buffaloes kutoka Zambia Opa alifunga bao moja na ndipo alipochaguliwa mchezaji bora wa mechi.
Advertisement
Tayari Opa pamoja na Simba Queens wamewasili salama jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kutoka Morocco ambapo tumeshika nafasi ya nne kwenye michuano hiyo.