Majaribio hayo yatakuwa ya mwezi mmoja na endapo atafanya vizuri Kayserispor watakuja mezani kujadiliana nasi kabla ya kumsajili moja kwa moja.
Baada ya kupata nafasi hiyo, Opa ameushukuru uongozi wa klabu kwa kumkubalia kwenda kufanya majaribio na anaamini ndoto zake za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi inatimia.
"Naushukuru uongozi wa klabu kwa kuniruhusu kwenda kufanya majaribio. Ndoto yangu ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi pia nataka kuwa balozi mzuri wa Simba na nchi kwa ujumla kama nitafanikiwa," amesema Opa.
Kama Opa atafanya vizuri na kufanikiwa kufuzu majaribio atakuwa mchezaji wa nne kutoka kikosi chetu kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi baada ya Mwanahamisi Omary anayekipiga nchini Morocco, Ruth Kipoyi na Flavian Mawete ambao wote wapo Uturuki.