Opa alifunga bao la kwanza dakika ya 18 kwa shuti kali baada ya shuti la mlinzi wa kushoto Dotto Evarist kuzuiwa na walinzi wa Mkwawa kabla ya kumkuta.
Baada ya bao hilo tuliendelea kulishambulia lango la Mkwawa huku wao wakifanya mashambulizi machache lakini hata hivyo hatukuweza kubadili matokeo.
Opa alitupatia bao la pili dakika ya 57 baada ya shuti la kiungo mshambuliaji Pambani Kuzoya kupanguliwa na mlinda wa Mkwawa na yeye kumalizia.
Advertisement
Hata hivyo Opa alikuwa na nafasi ya kupiga hat trick baada ya kukosa mkwaju penati mwishoni mwa kipindi cha pili.
Ushindi wa leo unatufanya kufikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi tano ambapo mchezo unaofuata utakuwa dhidi ya Amani Queens utakaopigwa Januari 18.