Mlinzi wa kati Joash Onyango, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month) baada ya kuwashinda mlinda mlango Aishi Manula na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone.
Onyango raia wa Kenya anakuwa mchezaji wa pili kunyakua tuzo hiyo tangu ilipoanza kudhaminiwa na kampuni Februari mwaka huu, ambapo Miquissone alishinda.
Pamoja na tuzo hiyo pia Onyango atakabidhiwa fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka Emirate Aluminum.
Mshindi wa tuzo hiyo hupatikana baada ya Kamati Maalumu kupitisha wachezaji watano ambao wamefanya vizuri zaidi kwa mwezi husika na kuwachuja hadi watatu ambao wanaingia fainali na kupigiwa kura moja kwa moja na mashabiki kupitia Tovuti hii.
Mchanganuo wa kura zilivyopigwa:
Jumla ya Kura ni 25,719
Onyango Kura 20,288 Asilimia 79
Manula Kura 4673 Asilimia 18
Miquissone Kura 758 Asillimia 2